MAMBO10 Y A KUSHANGAZA AMBAYO WAWEZAFANYA UKIWA #GOOGLE

image

Google Inc ni moja kati ya
kampuni nguli na tajiri sana
mtandaoni. Google inapenda
sana kucheza na vitu na
kubuni mambo mapya kupitia
vitu hivyo hasa kiteknolojia.
inasemekana pengine ndio
kampuni kubwa ya kiteknolojia
inayoongoza kwa ubunifu.
Licha ya kuwa mafanikio
makubwa kampuni hii ina
mambo mbalimbali yanayovutia
na kufurahisaha. Leo
tutakuonesha baadhi ya
mambo ya kufurahisha
unavyoweza kuvifanya kupitia
Google Search.
Pia logo yake kwenye ukurusa
wa Google dot com huwa
inabadililika lakini kwa leo
hatutaeliweka hili, leo
tunakuonesha mambo kumi
unayoweza fanya ukiwa Google
dot com na kompyuta yako na
mengine ata kwenye simu
yako.

1. FANYA PAGE IZUNGUKE
KAMA PIPA
Ukiingia katika ukurasa wa
google na ukitafuta ‘DO A
BARREL ROLL’ page yote
itazunguka nyuzi 360

2. GOOGLE YA MWAKA 1998
Ukitaka ona jinsi google
ilivyokua mwaka 1998 basi
tafuta ‘ GOOGLE IN 1998 ‘
katika ukurasa wa google na
utaona muonekano wake kwa
mwaka huo jinsi ulivyokuwa
3. ATARI BREAKOUT
Katika ukurasa wa Google
tafuta ‘ ATARI BREAKOUT ‘ kisha
yatatokea majibu baada ya
hapo bonyeza ‘IMAGES’
litatokea gemu la kubomoa
matofari kwa kutumia ki mpira
kidogo unaweza ukalicheza
gemu hili.

4. ZERG RUSH
Ukiandika neno ‘ZERG RUSH‘
katika ukurasa wa google ,
yatakuja majibu vizuri kisa
utashangaa vinatokea vi O
vingi viingi chini na juu ya
kompyuta. vitaanza kula
maneno yote yaliyo jitokeza
katika hiyo page kama majibu.
ili kuviua vi O hivi inabidi
uvibonyeze na Mouse mara 3
kwa mkupuo

5. MVUTONO
Katika Sehemu ya kutafuta vitu
katika page ya google andika
‘Google Gravity’ kisha
bonyeza ‘I’m Feeling Lucky’
ukisogeza Mouse tuu utaona
maneno yaanza kudondoka
chini ya skrini yako kuonyesha
nguvu za mvutano

6. JIPANGIE MUDA/DAKIKA
Hii pia inavutia. hivi unajua
unaweza kujipangia muda
katika ukurasa wa google? ndio
unaweza mfano ukiandika ‘SET
TIMER FOR 10:30PM ‘
inamaanisha hapa ikifika saa
nne na nusu usiku kompyuta
yako itapiga kelele/mlio
kukukumbusha kuwa mda huo
umefika, kama alarm/kengere
tuu sio?

7. TAFUTA KWA SAUTI/
KUTAMKA
Sio lazima kila unachokitafuta
lazima ukiandike, unaweza pia
ukakitafuta kwa kutumia sauti
yako. jinsi ya kufanya hvyo,
Ingia katika ukurasa wa google
alafu tafuta kialama cha kipaza
sauti, mara nyingi kinakua
mwishoni mwa upande wa
kulia katika sehemu
unayoandika kitu unachotaka
kukitafutakibonyeze kile kisha
unaweza sema kitu unachotaka
kukitafuta.

8. VITABU
Kama wewe ni mpenzi sana wa
vitabu na unapenda soma basi
kuna njia rahisi ya kuvipata.
Ingia google sehemu ya
kutafuta, Andika ‘ BOOKS BY ‘
kisha jina la mwandishi au
mtunzi, Hapo vitatokea vitabu
vyo vya huyo mwandishi/
mtunzi

9 .SINEMA
Ukiachana na vitabu, je wewe
ni mpenzi wa sinema? basi hili
litakusaidia pia. ingia ukurasa
wa google kisha andika jina la
mwigizaji ikifuatiwa na neno
‘MOVIES‘ hapo zitatikea
sinema za huyo msanii kisha
utachagua chaguo lako

10. GOOGLE KAMA KIOO
Hii pia ni ya kushangaza,
Google inaweza kuwa kama
kioo. hii inamaanisha
ukiandika maneno yatakua
yanaonekana kama yako ndani
ya kioo yaani yatakua
yamejigeuza, yanaanza kulia
yanaenda kushoto. kuona
mfumo huu wa kioo bofya hapa
Hayo ndio mambo 10 ambayo
unaweza fanya ukiwa katika
tovuti ya http://www.google.com kwa
kumpyuta na mengine ata
kwenye simu-janja, mambo
haya ni ya aina yake na ya
kushangaza kwa sababu tovuti
nyingi hazina ubunifu kama
huu. Google bado ipo katika
zile kampuni zenye maendeleo
sana katika masuala ya
teknolojia na inatoa
changamoto kwa makampuni
mengine kama Apple.

MHARIRI:

image

Ambuli Victor

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s