APP YA WIKI: #LEANDROID

image

Programu ya LeanDroid ya
Androidi ni appu moja ya aina
yake. Kazi yake ni rahisi –
kurefusha maisha ya chaji yako
kwenye simu na kukufanya
usisumbuke kuwasha na
kuzima intaneti.

Unaweza usiamini kusikia hii
bila maelezo ila maelezo yake
ni marahisi na madogo kama
programu yenyewe: Hivi
ndivyo LeanDroid inavyofanya
kazi:

1. Unapofunga
skrini, inasubiri
dakika kadhaa
(utazoamua
wewe) alafu
inakata intaneti
kukurefushia
chaji.

2. Leandroid
itawasha
intanetikila
baada ya saa
moja (ukiamua)
kuruhusu
WhatsApp na
programu
nyingine
kutumia intaneti
kwa dakika moja
kisha itazima
intaneti tena.

3. Utakapofungua
skrini na kuanza
kutumia simu,
itawasha
intaneti kwa
raha zako.

image

Unaamini sasa?

Chaguzo za LeanDroid
Zaidi ya kukurahisishia kwa
namna hii,
LeanDroid imetengenezwa
kutoingiliana na kazi zako pale
unapokuwa unashusha kitu au
umeunga simu na simu
nyingine au kompyuta
(tethering) au kama umejiunga
na wayalesi. Pia inaweza
kuacha intaneti iwe imewaka
wakati unachaji kwa umeme
moja-kwa-moja lakini unaweza
kuchagua ikate intaneti wakati
inachaji kwa kompyuta ili ipate
chaji haraka. Chaguzo nyingne
ni zile zinazohusu ‘bluetooth’
na unaweza kujipatia uhuru
zaidi wa kucheza na chaguzo
zingine kama utaamua kuilipia
programu hiyo. Unaweza kuona
chaguzo hizi zote hapa kwenye
hii picha chini.

Ukiangalia kwenye soko la
Google Play hauwezi kupata
programu nyingine ndogo
(248kb kuishusha/ 2.8MB
kwenye RAM), rahisi kutumia
na bure inayofanya kazi vyema
kama LeanDroid kwa sasa.

Programu hii inastahili kuwa
App ya leo – jipatie hapa au
mshirikishe mwenzio – >> Soko
la Google Play

MHARIRI:

image

Ambuli Victor

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s