APPS KUMI MUHIMU KWA SIMU YAKO YA NOKIA ASHA

image

Simu za Nokia Asha ni moja ya
simu maarufu na zilizouzika zaidi
kutoka Nokia kwa miaka yake ya
mwishoni kabla ya kampuni hiyo
kununuliwa na Microsoft na
zinaendelea kuuzika vizuri ata
baada ya kuwa chini ya Microsoft.
Kwenye mipangilio ya familia za
simu kulingana na uwezo wake
kuna simu za kawaida, alafu kuna
simu zinazoitwa ‘featured phones’
kisha zinafuata simu-janja
(smartphones).
Simu za Nokia Asha nyingi zinaingia
kwenye familia a ‘featured phones’,
hii ikimaanisha ni simu zenye uwezo
wa kiwango cha kawaida hii ikiwa ni
pamoja na uwezo wa kupokea apps
mpya, kutumia intaneti pamoja na
mambo mengine mengi kama vile
kuwa na kamera. Tofauti yake kubwa
na simu-janja ni pamoja na kuwa
simu-janja zinauwezo mkubwa zaidi
wa kupokea apps zenye ukubwa zaidi
na ata kiutendaji kazi zinakuwa na
vitu kama RAM, prosesa na diski-
uhifadhi wa kiwango cha juu zaidi
kulinganisha na ‘featured phones’.
Ingawa familia ya simu za Nokia
Asha zinawekwa kwenye kundi la
‘feautured’ bado inauwezo mzuri kwa
matumizi ya kila siku ya kawaida, na
kupitia ushirikiano na watengenezaji
wa apps kuna apps mbalimbali
zimetengenezwa kwa ajili ya simu
hizi ili angalia kukufanya
kutosononeka utamu wanaoupata
watumiaji wa simu zenye Android au
zile za iPhone kwa wingi apps
walionao. Na hapa leo tumekuletea
baadhi ya apps muhimu zaidi kuwa
nazo kwa matumizi ya kawaida ya
kila siku;
WhatsApp S40
WhatsApp ni moja ya app muhimu
kabisa siku hizi kwa ajili ya
mawasiliano. Hii inakuwezesha
kuchati na marafiki wa nchini na nje
ya nchi kwa uraisi kabisa, unaweza
ipata kwa kubofya hapa – http://
store.ovi.com/content/172049
CNN
Je unapenda kujua kinachotokea
ulimwenguni kila siku? Ni muhimu!
Kupitia app ya CNN pata habari
mbalimbali za ulimwenguni kupitia
simu yako. Bofya kuipata – http://
store.ovi.com/content/212837
Video HD
Je kuna video ya mwanamuziki mpya
imetoka na upo mbali na kompyuta?
App ya Video HD inakuwezesha
kutazama video kutoka mtandao wa
YouTube, tena kwa kiwango cha HD.
Kuipakua – http://store.ovi.com/
content/161242
Editori PDF
Fungua na soma mafaili ya pdf kwa
uraisi kwenye simu yako. Kwa mafaili
makubwa sana app hii inaweza
chukua muda kidogo kuyafungua ila
mwish0 wa huo muda utaweza
kuyasoma kwa uzuri tuu. Kuipakua –
http://store.ovi.com/content/363956
Opera Mini Web Browser
Ulimwengu wa simu za ‘featured’
ungekuwaje bila Opera Mini? Mgumu
kweli kweli! Tokea enzi za miaka ile
kabla simu janja hazijaenea na kuwa
bei rahisi ni Opera Mini ndiyo
ilikuwa inatusaidia kutumia
mtandao, na inaendelea kubakia
bora. Kuipakua – http://
store.ovi.com/content/46870
Sophie Cam
Je wewe unapenda kupiga picha?
”Viselfizi’ vya hapa na pale? Basi
Sophie Cam itakufaa. Hii inakupa
uwezo wa kubadilisha muonekano wa
picha yako. Kuipakua – http://
store.ovi.com/content/212085
Wiki Encyclopedia
Kuelimika ni jambo zuri sana. Epuka
kujikuta unaitaji kufahamu jambo
flani kwa haraka alafu kuuliza kwa
watu ni soo au upo peke yako, hapo
ndio umuhimu wa app kama
Encyclopedia unakuja. App hii
inakusaidia kusaidia kufungua na
kusoma mtandao maarufu wa
WikiPedia kwa urahisi. Kuipakua –
http://store.ovi.com/content/202207
Viber
Viber ni app nyingine maarufu
duniani kwenye masuala ya kuchati.
Viber inasifika kwa kukuwezesha ata
kupigiana simu za bure na
mwenzako anyetumia app hiyo.
Kuipakua – http://store.ovi.com/
content/565945
Pocket Light Free
Umeme umezimika alafu hauna
tochi? Giza nene? App hii
inabadilisha kioo chako cha simu
cha LED kuwa tochi pale unaitaji
mwanga wa zaidi kuona kwenye giza.
Kuipakua – http://store.ovi.com/
content/289818
Facebook
Yes, mwishoni kabisa ni Facebook…
hii haitaji maelezo mengi sana…
Tunaielewa, ipakue kutoka hapa –
http://store.ovi.com/content/238066
Kwa leo ni hapo tuu, je kuna jambo
unataka lifahamu? Tuwasiliane
kupitia akaunti zetu za Facebook,
Twitter, Instagram au Google+
(Bofya kwenye jina kuungana nasi)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s