Wanajeshi wa Uingereza wakwama Nairobi

Tongola Mate

Image

{Picha – Maktaba}

NAIROBI, KENYA, Zaidi ya wanajeshi elfu moja wa Uingereza wamekwama hapa jijini Nairobi kufuatia mvutano wa kidiplomasia kati ya serikali ya Kenya na Uingereza.

Hii ni baada ya Kenya kudinda kutia upya sahini mkataba wa makubaliano na Uingereza, wa kuwaruhusu wanajeshi zaidi kuelekea eneo la Nanyuki kwa mafunzo.

Mvutano huo umehusishwa na ilani za usafiri za hivi majuzi zilizotolewa na Uingereza kwa raia wake kuzuru taifa hili. Aidha, duru zimearifu kwamba Kenya imetoa takwa la kuondolewa kwa ilani hiyo kabla ya kuwaruhusu wanajeshi hao kuelekea Nanyuki kwa mafunzo.

Msemaji wa ubalozi wa Uingereza nchini Stephen Burns amethibitisha kuwepo kwa mvutano huo na kuelezea imani yake kwamba utasuluhishwa hivi karibuni.

Hatua hii imesababisha kucheleweshwa kwa kundi jipya la wanajeshi waliopaswa kuwasili nchini baada ya kundi lingine kukamilisha mafunzo yao ya wiki 6 chini ya mpango ujilikanao kama British Armmy Training Unit in Kenya (BATUK).

View original post

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s